OFA MAALUM: KILA KITABU TSH 2,000/-.

Simple Online Income Skills (SOIS).
—————

Habari yako rafiki! Kama ilivyo kawaida yetu, hapa ni mahali pa kupata maarifa rahisi ya kuanza kunufaika kiuchumi/kibiashara mtandaoni bila kutumia nguvu nyingi sana. Leo nimekueletea ofa maalum, upate vitabu vyetu vya PDF kwa bei nafuu sana; yaani TSH 2,000 badala ya bei za kawaida, za vitabu hivyo (Tsh 2,500-7,000).

VITABU UTAKAVYOPATA HAPA NI:
1. Namna ya kutengeneza graphics kwa smartphone na kuziuza kupitia WhatsApp [Jinsi nilivyoanza na ninavyouza graphics rahisi mtandaoni].
2. Kuongeza upatikanaji wa wateja kupitia WhatsApp.
3. Namna ya kufungua blogu yako ndogo rahisi mwenyewe—kwa smartphone.
4. Unavyoweza kuuza maandishi yako mtandaoni.
5. Maarifa na uzoefu wako ni kipato chako mtandaoni.
6. Andika kwa mkono na uuzie mtandaoni.
7. Advanced Stationery Skills [Online Typing]: Kuandika kwa ajili ya wengine— mtandaoni.

Vitabu vyote vipo katika fomati ya PDF, na vinapatikana kupitia WhatsApp/e-mail; baada tu ya kufanya malipo kwa namba yetu ya M-pesa. Vilevile utaunganishwa kwenye kikundi cha whatsapp cha SIMPLE ONLINE INCOME SKILLS; kwa ajili ya kuwasilisha changamoto yako yoyote kisha kujibiwa.

Karibu.
Angalia makava ya vitabu hivyo, hapa chini kisha ingia Inbox kwetu kwa kugusa HAPA OPEN [INBOX DOOR], ILI UTUTAARIFU KITABU UNACHOHITAJI.
_________________
№1. Namna ya kutengeneza graphics kwa smartphone na kuziuza kupitia WhatsApp.
#1. UTANGULIZI KWA UFUPI: Hapa utapata maelekezo rahisi, kwa msaada wa picha za screenshot za hatua zote; namna ya kutengeneza graphics kwa kutumia smartphone. Graphics kama posters/flyers, kalenda, business card, makava rahisi ya vitabu na nyinginezo ili kuwahudumia wahitaji wa graphics hizo, wanaopatikana kwa urahisi kupitia WhatsApp. 
Wateja wako watakuwa wakituma maelekezo yao kwa WhatsApp, na baada ya wewe kukamilisha ubunifu huo, wanakulipa kwa mobile money; kama M-pesa, Halopesa, Airtel Money, Tigo Pesa, T-pesa n.k. wewe unawatumia kazi zao katika fomati za picha original/PDF—kwa whatsapp/e-mail.
_______________
_______________
№2. Kuongeza upatikanaji wa wateja kupitia WhatsApp.
#2. UTANGULIZI KWA UFUPI: Baada ya kusoma kitabu hiki utaweza kufanya mambo yafuatayo:
• Kukusanya na kuhifadhi (save) namba zote za washirika wote wa vikundi vyote vya whatsapp unavyojiunga. Utafanya hivi kwa haraka—ndani ya muda mfupi.
• Kuongeza watazamaji wengi wa status zako ndani ya muda mfupi.
• Ku-foward tangazo au ujumbe wako, kwenda kwa watu wengi ndani ya muda mfupi—kwa kutumia lebo (label) maalum.
• Kuweka mkakati wa kutengeneza uhakika wa wateja wengi tarajiwa wasio na kikomo—kupitia WhatsApp.
_______________
_______________
№3. Namna ya kufungua blogu yako ndogo rahisi mwenyewe—kwa smartphone.
#3. UTANGULIZI KWA UFUPI: Hapa utaweza kutumia smartphone yako, kufungua blogu yako ndogo rahisi ya bure; kwa kutumia majukwaa mawili ya mtandaoni: blogspot na WordPress.
Utafahamu hatua moja hadi nyingine. Jambo linalowezekana kufanyika ndani ya dakika chache sana.
_______________
_______________
№4. Unavyoweza kuuza maandishi yako mtandaoni.
#4. UTANGULIZI KWA UFUPI: Baada ya kusoma kitabu hiki utaweza kuuza maandishi ya maarifa yako au chochote unachotaka kuuuza katika fomati ya maandishi. Utajifunza jinsi ya kuanza kufanya hivyo kwa gharama ndogo sana, kiasi kwamba ni kama hakuna gharama. Ikiwa wewe ndiyo kwanza unaanza kuandika na haujajua wapi utaanzia kupata uzoefu wa awali, katika kuuza maandishi mtandaoni; hapa ni mahali sahihi. Ni kitabu kizuri na kina kurasa chache (38 tu) zenye mambo muhimu sana.
_______________
_______________
№5. Maarifa na uzoefu wako ni kipato chako mtandaoni.
#5. UTANGULIZI KWA UFUPI: Katika kitabu hiki, utajifunza namna ya kutengeneza mfumo rahisi sana wa kuuza maarifa ya uzoefu au taaluma yako. Kwa kuwa hivi sasa kuna watu wengi wanaopatikana WhatsApp, kitabu hiki kinakupa mwongozo wa namna nzurí ya kufungua na kuunganisha vizuri matumizi ya chaneli rahisi ya youtube, blogu rahisi ya bure na vikundi vya WhatsApp; vyenye wanafunzi wanaolipia kozi au mafunzo unayotoa.
_______________
_______________
№6. Andika kwa mkono na uuzie mtandaoni.
#6. UTANGULIZI KWA UFUPI: Pengine umejiuliza 'nawezaje kuuzia mtandaoni, maandishi niliyoyaandika kwa mkono?'. Jibu ni kwamba: jambo hilo linawezekana. Katika kitabu hiki utafahamu namna ya kuandika maandishi yako kwenye karatasi ambazo zitafanyiwa scanning kwa kutumia smartphone, na kuzitumia picha kama kurasa (pages) za PDF kwa mpangilio mzuri. Hapa utaweza kutengeneza dokumenti fupi fupi zenye mwonekano mzuri. Jambo lina matokeo mazuri sana kwa watu wenye mwandiko mzuri, kwenye maandishi yao ya mkono. 
Je, unafahamu kuwa watu wengi hivi sasa, bado wanapenda sana kusoma maandishi yaliyoandikwa kwa mwandiko wa mkono? Ndiyo, ukiwa na mwandiko mzuri, na unao uwezo mzuri kwenye somo au taaluma fulani unaweza kuweka mambo hayo kwenye maandishi na kisha kuuza kwa namna hiyo.
Utajifunza vilevile namna ya kuwataarifu watu wengi waliopo WhatsApp, kuhusu uwepo wa dokumenti zako.
_______________
_______________
№7. Advanced Stationery Skills [Online Typing]: Kuandika kwa ajili ya wengine— mtandaoni.
#7. UTANGULIZI KWA UFUPI: Katika kitabu hiki chenye kurasa chache (55). Utajifunza namna ya kulipwa kwa kuandika kazi mbalimbali za maandishi, kwa ajili ya wengine—mtandaoni (Online Typing). Watu wengi wanahitaji kupata kazi zao fulani katika maandishi, lakini hawana muda wa kutosha kufanya hivyo. 
Kuna watu wengi wanahitaji ku-type risala, mashairi/nyimbo, hotuba, kazi za masomo (assignments) na nyingine nyingi. Pia wengine wanatamani kuzibadili audio fulani (kama mahubiri, semina na mihadhara), kuwa kwenye maandishi au vitabu. Ukisoma kitabu hiki, utaweza kutumia smartphone yako kufanikisha kazi hizi kwa urahisi—kuliko unavyodhani. 
Wateja wako watakulipa kwa Mobile money au mifumo mingine ya kupokea malipo kwenye intaneti (ikiwa wapo nchi nyingine za nje). Wewe utawapatia kazi zao katika fomati za kielektroniki (softcopy); kwa WhatsApp/e-mail.
_______________
Karibu sana.
EMMANUEL KIMANISHA.


Comments

Popular Posts